MWISHO WA SIRI, DENNIS SHONKO

𝕄𝕨𝕚𝕤𝕙𝕠 𝕨𝕒 𝕊𝕚𝕣𝕚
𝐃𝐞𝐧𝐧𝐢𝐬 𝐒𝐡𝐨𝐧𝐤𝐨

Mwisho wa Siri na Dennis Shonko

𝓜𝓴𝓲𝓽𝓮𝓷𝓭𝓪𝓷𝓪 𝓳𝓪𝓶𝓪𝓷𝓲, 𝓵𝓲𝓵𝓸 𝓱𝓲𝓵𝓸 𝓽𝔀𝓪𝓵𝓲𝓼𝓸𝓶𝓪,
𝓢𝓲𝓴𝓾 𝓶𝓸𝓳𝓪 𝓾𝓴𝓾𝓫𝔀𝓪𝓷𝓲, 𝔀𝓪 𝓴𝓾𝓹𝓲𝓷𝓰𝓪 𝓽𝓪𝓼𝓲𝓶𝓪𝓶𝓪?
𝓦𝓮𝓷𝓰𝓲 𝓽𝓾𝓹𝓸 𝓶𝓲𝓰𝓸𝓷𝓰𝓸𝓷𝓲, 𝓿𝓲𝓼𝓸𝓰𝓸 𝓽𝔀𝓪𝓿𝓲𝓽𝓪𝔃𝓪𝓶𝓪,
𝓣𝓾𝓱𝓲𝓯𝓪𝓭𝓱𝓲 𝓪𝓴𝓲𝓵𝓲𝓷𝓲, 𝔀𝓪𝓷𝓮𝓷𝓾 𝓽𝓾𝔀𝓮 𝓼𝓪𝓵𝓪𝓶𝓪,
𝓢𝓲𝓬𝓱𝓸𝓴𝓲 𝓴𝓾𝔀𝓪𝓾𝓵𝓲𝔃𝓪, 𝓾𝓴𝓾𝓫𝔀𝓪𝓷𝓲 𝓽𝓾𝔀𝓪𝓲𝓰𝓮?

“ᴋᴀᴛɪᴛɪʀᴏ, ᴋᴏᴍᴀ ᴋᴜᴡᴀᴘɪɢᴀ ᴘɪᴄʜᴀ ᴡᴀᴛᴜ ʜᴀᴡᴀ! ᴛᴜᴋɪᴋᴀᴍᴀᴛᴡᴀ ᴛᴜᴛᴀᴊᴜᴀ ᴋɪʟɪᴄʜᴏᴍᴛᴏᴀ ᴋᴀɴɢᴀ ᴍᴀɴʏᴏʏᴀ!”

ᴍᴡɪꜱʜᴏ ᴡᴀ ꜱɪʀɪ ɴɪ ʜᴀᴅɪᴛʜɪ ɪɴᴀʏᴏʟᴇɴɢᴀ ᴋᴜᴍʟᴇᴀ ᴍᴡᴀɴᴀꜰᴜɴᴢɪ ᴋᴀᴛɪᴋᴀ ᴍᴀɪꜱʜᴀ ʏᴀ ᴜᴢᴀʟᴇɴᴅᴏ, ᴜᴍᴏᴊᴀ, ᴜᴡᴀᴊɪʙɪᴋᴀᴊɪ, ᴜᴛᴜ, ᴜᴀᴅɪʟɪꜰᴜ, ʜᴇꜱʜɪᴍᴀ ɴᴀ ʙɪᴅɪɪ. ʙɪʟᴀ ꜱʜᴀᴋᴀ ɪᴛᴀᴡᴀꜱɪꜱɪᴍᴜᴀ ᴡᴀꜱᴏᴍᴀᴊɪ ᴡᴇɴʏᴇ ᴜᴍʀɪ ᴍᴋᴜʙᴡᴀ ɴᴀ ᴍᴅᴏɢᴏ.

𝐉𝐢𝐧𝐬𝐢 𝐲𝐚 𝐤𝐮𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐧𝐚𝐤𝐚𝐥𝐚: https://docs.google.com/forms/d/e/1FAIpQLSevptCrobZ9fI6eoh9kAvkK_cZjrrdWPdxSeZHe56MhADZLpQ/viewform?usp=sf_link

A SILENT SONG AND OTHER STORIES; EDITED BY GODWIN SIUNDU

A Silent Song and Other Stories edited by Godwin Siundu (Spotlight Publishers), an anthology of short stories, that replaces Memories Lost.

MWONGOZO WA MAUDHUI KATIKA TUNGO ZA MUYAKA BIN-HAJI.

Utangulizi. Muyaka bin Haji ni kiumbe wa kihistoria na msanii mkongwe katika historia ya usanii, miongoni mwa wasanii wa kabla ya karne ya ishirini. Muyaka alizaliwa mjini Mvita katika ukoo wa Myinyi Malindi, miongoni mwa koo kumi na mbili za Waswahili, na aliishi kati ya 1776-1840. Kitabaka,Muyaka alikuwa mtu wa wastani. Katika uhai wake, Muyaka […]

MWONGOZO WA MAUDHUI KATIKA TUNGO ZA MUYAKA BIN-HAJI.

Tanzanian Abdulrazak Gurnah wins 2021 Nobel Prize in literature

Born in Zanzibar and based in England, Gurnah is a professor at the University of Kent.

He has published 10 novels and a number of short stories. He is best known for his 1994 novel “Paradise”, set in colonial East Africa during World War I, which was shortlisted for the Booker Prize for Fiction.

Continue reading

Wimbi la Mabadiliko na Dennis Shonko

Ingia Mbele Nyuma ukutane na wahafidhina! Taifa kama hili hukombolewa vipi? Usaliti na uongo utakita mizizi hadi lini? Chungu cha siri kitavunjwa na nani? Mmm, hadi lini? Pata uhondo!

Mwaka wa 2016, mswada wa Wimbi la Mabadiliko ulikuwa miongoni mwa miswada bora katika Tuzo ya Fasihi ya Ubunifu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Ufaransa nchini Kenya, Kampuni ya Uchapishaji ya Spotlight na Kampuni ya Nation Media Group.

Kwa mengi zaidi: 0745 344 387.

Dennis Shonko kwenye Gazeti la Taifa Leo

@DennisShonko LALA PEMA PROF. KEN WALIBORA:  INGAWA UMEONDOKA, HUTAFUTIKA MOYONI MWANGU.

@DennisShonko LALA PEMA PROF. KEN WALIBORA: INGAWA UMEONDOKA, HUTAFUTIKA MOYONI MWANGU.

Ulikuwa uvumi tu! Ufifi!

IMG_20200415_141522

Jumanne usiku, kila nilipopenyepenya kwenye mitandao ya kijamii niliwaona wengi wakikutajataja. Walikutajataja kwa kile ambacho nilikataa kabisa kuamini. Wengi hatukuamini na hivyo kutugeuza wakosoaji. Tuliwaonya ‘kasuku’ dhidi ya uvumi kuwa ulikuwa umetangulia mbele ya haki. Ili nisiutese moyo wangu nilizima data hadi keshoye Jumatano, 15/4/2020. Nikawa ninachakura kwenye Twitter, Whatsapp na Facebook. ‘Uvumi’ ulikuwa umetamba kote. Sikutaka ya kukisiwa tena! Nilipoiwasha televisheni, duh! Stesheni ya NTV ilikuwa na maandishi haya kwenye kiwambo: 

Continue reading

@DennisShonko NILIVYODHALILISHWA KWA KUZUNGUMZA LUGHA YA KISWAHILI

interview

Mwalimu na wanafunzi ofisini.

Nakumbuka namna mvua ilikuwa inatunyeshea mchana kutwa tulipokuwa safarini (usiulize tulikuwa na nani. Hayo ni ya siku nyingine). Safari ya kutoka jijini Nairobi kuelekea eneo la *Kiduni. Usishangae kuwa kunyesha kwa mvua hiyo hakukuitia imani yangu baridi. Baridi iliyokusudia kutugeuza kuku aliyenyonyolewa chini ya pepo zitokazo pande zote duniani. Ninachojaribu kusema ni kwamba, nilikuwa katika safari ya kwenda kuonja kipande kingine cha maisha au bora niseme, kuandika ibara nyingine ya maisha yangu.

Baada ya saa kadhaa za kusumbuana na utingo, tulifika katika Chuo cha Ualimu cha *Nira. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia humo, sikwambii kufika Kiduni. Watu wachache walikuwa bado wamepiga foleni wakisubiri ima kusajiliwa rasmi chuoni au kuwashika mikono wana wao katika shughuli hiyo nzima. Nilijua sikuwa na kila kitu kilichokuwa kinahitajika; si vitabu si si idadi tosha ya pesa. Ile kauli ya ‘mtu hujikuna ajipatapo’, nilijua haingenifaa wakati kama huo. Nilikuwa kama mbuzi mbele ya hakimu chui! Hebu nisonge mbele kidogo… Continue reading

@DennisShonko UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

Kwa mwaka wa pili mfululizo, Tamasha ya Kiswahili iliandaliwa katika ukumbi wa Huduma ya Maktaba kwa Taifa nchini Kenya (Jumamosi, Oktoba 14, 2017) eneo la Buruburu. Ingawa sikubahatika  kuhudhuria tamasha yenyewe mwaka wa 2016, nilihabarishwa ilivyokuwa yakuigwa.

   Bw Almasi bin Ndangili—ambaye ndiye aliyeibuka na wazo la kuwapo tamasha kama hiyo, ndiye aliyenipa mwaliko. Sawa na wapenzi wengine wa lugha ya Kiswahili, nilifika mapema ukumbini licha ya kukanyaga chechele hapa na pale safarini nikiwa na mwalimu mwenzangu, Peter. Baada ya kitambo kifupi, Bw Ndangili aliyekuwa mratibu na mshereheshaji wa hafla na mwandishi wa tamthilia ya Kifo cha Mwandisi Mmachinga iliyoigizwa hapo baadaye, aliifungua warsha. Stacy alituongoza katika kuuimba wimbo wa taifa. Baadhi ya majina yakutajika yalitambulishwa kwetu k.v Swaleh Mdoe, Bi Pauline Kea, Daktari Hamisi Babusa na Profesa Kineene wa Mutiso waliokuwa wamefika mle. Continue reading

Ngulamu Mwaviro ndiye mshindi wa Tuzo ya Ubunifu 2016 miongoni mwa Miswada 86

1f

Kumi na tano bora na wadhamini ya Tuzo ya Ubunifu

Tarehe 26/04/2017 ilikuwa siku ambayo mwanahabari  Ngulamu Mwaviro (Wa shirika la utangazaji la kitaifa-KBC) alitangazwa mshindi wa Tuzo ya Ubunifu ya 2016 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi  wa Alliance Francais jijini Nairobi.   Novela yake ya “Mkamia Maji” iliibuka mswada bora miongoni mwa themanini na sita (86) iliyokuwa imetumwa na waandishi chipukizi kutoka pembe zote nchini Kenya.

Akitoa hotuba yake fupi punde alipotangazwa mshindi, Mwaviro alisema kuwa hakutarajia hilo licha ya kuwa aliamini alikuwa ameufanyia kazi mswada huo ipasavyo. “Mswada huu ni jiwe lililokataliwa na mwashi . Kuna matbaa iliyokataa mswada huu na nikaona nijaribu bahati katika Tuzo ya Ubunifu,” aliongeza. Aidha, aliwamshukuru Mungu na kuwapongeza washiriki wote.” Kando na kutunukiwa shilingi milioni moja, mswada huo utachapishwa na Matbaa ya Sportlight na kisha uchapishwe ka Kifaransa. Continue reading

Tumbo Lisiloshiba-Alifa Chokocho na Dumu Kayanda

Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine ni mkusanyo wa hadithi fupi zilizoandikwa na waandishi waliobobea na wale wanaochipuka katika uandishi wa utanzu wa hadithi fupi. Hadithi katika mkusanyo huu zimeandikwa kwa ubunifu na kwa kuzingatia maswala ibuka katika jamii inayokwenda na utandawazi na usasaleo. Mkusanyo huu unaangazia maudhui mbalimbali kama vile: siasa, dini, ulemavu, masuala ya kijinsia, elimu, ukware, ulaghai, uchumi, mazingira, umaskini, uongozi, ukabila, mapenzi, ndoa, ushirikina miongoni mwa mengine. Masuala yaliyoshughulikiwa katika mkusanyo huu yataibua ilhamu ya msomaji, msomi, mtafiti na wanafunzi katika maisha yao. Maudhui, mtindo, lugha na uhusika ni viungo vilivyosukwa kwa namna ya kipekee katika mkusanyo huu.  Continue reading

Haini na Adam Shafi

Haini na Adam Shafi

Haini na Adam Shafi

Hamza, kijana mwandishi wa habari, anakamatwa kwa kutuhumiwa kuwa haini, hasa kutokana na uhusiano wake wa karibu na Hamduni, ambaye amempiga risasi na kumwua Kigogo, kiongozi wa nchi.

Sehemu kubwa ya riwaya hii inasimuliwa gerezani ambako Hamza pamoja na wengine waliosombwa na kurundikwa huko, wanateswa, kuthakilishwa na kutendewa unyama wa kila namna.Haini ni riwaya inayochukua tukio la kihistoria la kuuawa kwa kiongozi mmoja wa Kiafrika mwaka 1972, na kulifanya kiini cha kuyachunguza matatizo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ya nchi za Kiafrika baada ya uhuru, chini ya mifumo ya utawala inayojali tu maslahi ya wachache. Continue reading

Kasri ya Mwinyi Faud na Adam Shafi Adam

Kasri ya Mwinyi Faud na Adam Shafi Adam

Kasri ya Mwinyi Faud na Adam Shafi Adam

Kasri ya Mwinyi Fuad ni mojawapo wa riwaya maarufu katika fasihi ya Kiswahili. Hii ni riwaya inayosawiri mvutano baina ya ubwana na umwinyi kwa upande mmoj a na unyonge na utwana kwa upande wa pili.
Continue reading