Tamthilia ya ‘AMEZIDI’ na Said A. Mohamed
Ame na Zidi wanajikuta katika umaskini mkubwa katika bahari iliyohaa mali. Katika hali hii ya uhitaji, wanatambua kuwa hawana jingine la kufanya ila kuomba msaada ili wayatosheleze mahitaji yao. Msaada unapokuja, unaleta unaleta madhara mengi zaidi.
Huu ni mchezo mawazoni unaotazama matatizo ya kijamii na ya kiuchumi katika nchi nyingi za kiafrika za hivi leo.
Mwandishi alizaliwa Unguja (Zanzibar) mwaka wa 1947. Alielimishwa huko huko Unguja na baadaye akajiunga na chuo kikuu cha Dar-es- Salaam, na kisha chuo kikuu cha Leipzig, Ujerumani. Amefundisha katika shule za upili na vyuo mbalimbali. Kabla ya ku7hamia Ujerumani, alikuwa Profesa katika Chuo kikuu cha masomo ya kigeni cha Osaka, Ujapani. Continue reading →
Please Share this post | Wajulishe na wengine pia