Tamthilia ya Mtahiki Meya – Timothy M.Arege

SEHEMU I

Onyesho I.

Mstahiki Meya

Mstahiki Meya

Mchezo uanzapo, tunakutana na Waridi ambaye ni nesi na Siki ambaye ni daktari. Wote wawili wako kwenye zahanati ya Jiji. Daktari Siki anaonekana mwenye kusumbuliwa na jambo fulani; pengine matatizo ya ukosefu wa dawa zahanatini. Waridi aingiapo, wanaanza kuangazia swala la ukosefu wa dawa kwenye zahanati.

Waridi anamwambia Siki kwamba, shehena ya dawa iko bahari kuu na kwamba ingewasili baada ya siku tatu. Hii ni kwa mujibu wa Mstahiki Meya mweneyewe.

Zahanati ingepokea dawa hizo baada ya siku tatu zingine baada ya kuwasili nchini. Meya anasema wagonjwa wasubiri dawa, naye daktari anashangaa kana kwamba ugonjwa nao utasubiri.

Kutokana na mazungumzo ya Waridi na daktari Siki tunagundua kwamba, zaidi ya kukosekana kwa dawa, wagonjwa hawana pesa za kulipia huduma za matibabu. Hata hivyo, amri ni kwamba, lazima wagonjwa walipie huduma za afya kabla hazijatolewa kwao. Waridi anatetea hali hii kwa kusema kwamba nchi yao ni maskini.

Siki anapomuuliza mwenye kusema kwamba nchi ni maskini, Waridi anasema kwamba ameyasikia tu maneno hayo kutoka kwa wanasiasa, vyombo vya habari na wasomi. Siki haelekei kukubaliana naye na anashangaa kwamba ‘ameyasikia tu’. (Hii inadhihirishwa kwamba, vyombo vya habari, wanasias na wasomi wanawapotosha wananchi kwamba nchi yao ni maskini.) Pindi anaingia mama mwenye mtoto mgonjwa. Waridi anamkemea lakini Siki anampokea na kuanza kumhudumia. Continue reading