Dennis Shonko kwenye Gazeti la Taifa Leo

@DennisShonko NILIVYODHALILISHWA KWA KUZUNGUMZA LUGHA YA KISWAHILI

interview

Mwalimu na wanafunzi ofisini.

Nakumbuka namna mvua ilikuwa inatunyeshea mchana kutwa tulipokuwa safarini (usiulize tulikuwa na nani. Hayo ni ya siku nyingine). Safari ya kutoka jijini Nairobi kuelekea eneo la *Kiduni. Usishangae kuwa kunyesha kwa mvua hiyo hakukuitia imani yangu baridi. Baridi iliyokusudia kutugeuza kuku aliyenyonyolewa chini ya pepo zitokazo pande zote duniani. Ninachojaribu kusema ni kwamba, nilikuwa katika safari ya kwenda kuonja kipande kingine cha maisha au bora niseme, kuandika ibara nyingine ya maisha yangu.

Baada ya saa kadhaa za kusumbuana na utingo, tulifika katika Chuo cha Ualimu cha *Nira. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia humo, sikwambii kufika Kiduni. Watu wachache walikuwa bado wamepiga foleni wakisubiri ima kusajiliwa rasmi chuoni au kuwashika mikono wana wao katika shughuli hiyo nzima. Nilijua sikuwa na kila kitu kilichokuwa kinahitajika; si vitabu si si idadi tosha ya pesa. Ile kauli ya ‘mtu hujikuna ajipatapo’, nilijua haingenifaa wakati kama huo. Nilikuwa kama mbuzi mbele ya hakimu chui! Hebu nisonge mbele kidogo… Continue reading

NASIKIA SAUTI YA MAMA – Tawasifu ya Prof. Ken Walibora

Baada ya tamthilia yake ya pili [MBAYA WETU] kuingia madukani, Prof. Ken Walibora ‘kaibua kitabu kinachoeleza safari ya maisha yake ilovyouwa na inavyozidi kuwa kila jua linapochomoza.

Uketo wa Lugha

“Nasikia Sauti ya Mama” ina uketo wa lugha ya kiswahili inayodhihirisha ukwasi al’onao profesa Ken na mno, weledi wake wa kuyaeleza mengi kwa njia ya kusisimua hivyo kumnata msomaji.

………

Heko kwa wanalonghorn Publishers kwa kujitoma katika hili la tawasifu: NASIKIA SAUTI YA MAMA (Ken Walibora) na “MBALI NA NYUMBANI (Adam Shafi) ni tuzo bora kwetu sote!

NASIKIA SAUTI YA MAMA - Tawasifu ya Prof. Ken Walibora

NASIKIA SAUTI YA MAMA – Tawasifu ya Prof. Ken Walibora

Continue reading

KOPO LA MWISHO NA HADITHI NYINGINE –OMAR BABU (Mhariri)

KOPO LA MWISHO NA HADITHI NYINGINE –OMAR BABU (Mhariri)

KOPO LA MWISHO NA HADITHI NYINGINE –OMAR BABU (Mhariri)

Kopo la mwisho na hadithi nyingine ni mkusanyiko wa hadithi ambazo zimepigwa msasa tena kwa makini naye Omar Babu [Abu Marjan] ambaye ni mshairi na mwandishi wa riwaya na hadithi fupi.

Ni diwani inayoshughulikia maudhui tofautitofauti; Ukabila, siasa. Elimu, mapenzi n.k  … “Ni hadithi zinazoandama mtindo sahili na zinazoashiria masuala yanayomkabili binadamu.”

Kopo la mwisho na hadithi nyingine

Continue reading

KAMUSI TEULE ya Kiswahili – Kilele cha Lugha; East African Publishers Ltd.

KAMUSI TEULE ya Kiswahili - Kilele cha Lugha; East African Publishers   Ltd.

KAMUSI TEULE ya Kiswahili – Kilele cha Lugha; East African Publishers Ltd.

Yapo makamusi na kamusi ambazo hazikomi kuchapishwa kila uchao; Hili ni
jambo la kupendeza na la kufurahikia maana’ke, inaashiria kesho njema
yenye utajiri wa mengi katika lugha ya Kiswahili.

KAMUSI TEULE ya Kiswahili – Kilele cha Lugha

“Ni zao la utafiti wa kina uliofanywa na waandishi na wanaleksikogrofia
wenye tajriba kubwa. Continue reading

Shreds of Tenderness By John Ruganda

Shreds of Tenderness By John Ruganda

Shreds of Tenderness By John Ruganda

Shreds of Tenderness is a heart-rending, masterfully crafted play which is replete with shocking revelations and reversals.

Not Long ago, a tyrant took over the reins of Government and unleashed terror throughout the Motherland. Wak fled. Continue reading