Kwa mwaka wa pili mfululizo, Tamasha ya Kiswahili iliandaliwa katika ukumbi wa Huduma ya Maktaba kwa Taifa nchini Kenya (Jumamosi, Oktoba 14, 2017) eneo la Buruburu. Ingawa sikubahatika kuhudhuria tamasha yenyewe mwaka wa 2016, nilihabarishwa ilivyokuwa yakuigwa.
Bw Almasi bin Ndangili—ambaye ndiye aliyeibuka na wazo la kuwapo tamasha kama hiyo, ndiye aliyenipa mwaliko. Sawa na wapenzi wengine wa lugha ya Kiswahili, nilifika mapema ukumbini licha ya kukanyaga chechele hapa na pale safarini nikiwa na mwalimu mwenzangu, Peter. Baada ya kitambo kifupi, Bw Ndangili aliyekuwa mratibu na mshereheshaji wa hafla na mwandishi wa tamthilia ya Kifo cha Mwandisi Mmachinga iliyoigizwa hapo baadaye, aliifungua warsha. Stacy alituongoza katika kuuimba wimbo wa taifa. Baadhi ya majina yakutajika yalitambulishwa kwetu k.v Swaleh Mdoe, Bi Pauline Kea, Daktari Hamisi Babusa na Profesa Kineene wa Mutiso waliokuwa wamefika mle. Continue reading