Haini na Adam Shafi

Haini na Adam Shafi

Haini na Adam Shafi

Hamza, kijana mwandishi wa habari, anakamatwa kwa kutuhumiwa kuwa haini, hasa kutokana na uhusiano wake wa karibu na Hamduni, ambaye amempiga risasi na kumwua Kigogo, kiongozi wa nchi.

Sehemu kubwa ya riwaya hii inasimuliwa gerezani ambako Hamza pamoja na wengine waliosombwa na kurundikwa huko, wanateswa, kuthakilishwa na kutendewa unyama wa kila namna.Haini ni riwaya inayochukua tukio la kihistoria la kuuawa kwa kiongozi mmoja wa Kiafrika mwaka 1972, na kulifanya kiini cha kuyachunguza matatizo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi ya nchi za Kiafrika baada ya uhuru, chini ya mifumo ya utawala inayojali tu maslahi ya wachache. Continue reading