Wimbi la Mabadiliko na Dennis Shonko

Ingia Mbele Nyuma ukutane na wahafidhina! Taifa kama hili hukombolewa vipi? Usaliti na uongo utakita mizizi hadi lini? Chungu cha siri kitavunjwa na nani? Mmm, hadi lini? Pata uhondo!

Mwaka wa 2016, mswada wa Wimbi la Mabadiliko ulikuwa miongoni mwa miswada bora katika Tuzo ya Fasihi ya Ubunifu iliyodhaminiwa na Ubalozi wa Ufaransa nchini Kenya, Kampuni ya Uchapishaji ya Spotlight na Kampuni ya Nation Media Group.

Kwa mengi zaidi: 0745 344 387.

Dennis Shonko kwenye Gazeti la Taifa Leo

@DennisShonko LALA PEMA PROF. KEN WALIBORA:  INGAWA UMEONDOKA, HUTAFUTIKA MOYONI MWANGU.

@DennisShonko LALA PEMA PROF. KEN WALIBORA: INGAWA UMEONDOKA, HUTAFUTIKA MOYONI MWANGU.

Ulikuwa uvumi tu! Ufifi!

IMG_20200415_141522

Jumanne usiku, kila nilipopenyepenya kwenye mitandao ya kijamii niliwaona wengi wakikutajataja. Walikutajataja kwa kile ambacho nilikataa kabisa kuamini. Wengi hatukuamini na hivyo kutugeuza wakosoaji. Tuliwaonya ‘kasuku’ dhidi ya uvumi kuwa ulikuwa umetangulia mbele ya haki. Ili nisiutese moyo wangu nilizima data hadi keshoye Jumatano, 15/4/2020. Nikawa ninachakura kwenye Twitter, Whatsapp na Facebook. ‘Uvumi’ ulikuwa umetamba kote. Sikutaka ya kukisiwa tena! Nilipoiwasha televisheni, duh! Stesheni ya NTV ilikuwa na maandishi haya kwenye kiwambo: 

Continue reading

@DennisShonko NILIVYODHALILISHWA KWA KUZUNGUMZA LUGHA YA KISWAHILI

interview

Mwalimu na wanafunzi ofisini.

Nakumbuka namna mvua ilikuwa inatunyeshea mchana kutwa tulipokuwa safarini (usiulize tulikuwa na nani. Hayo ni ya siku nyingine). Safari ya kutoka jijini Nairobi kuelekea eneo la *Kiduni. Usishangae kuwa kunyesha kwa mvua hiyo hakukuitia imani yangu baridi. Baridi iliyokusudia kutugeuza kuku aliyenyonyolewa chini ya pepo zitokazo pande zote duniani. Ninachojaribu kusema ni kwamba, nilikuwa katika safari ya kwenda kuonja kipande kingine cha maisha au bora niseme, kuandika ibara nyingine ya maisha yangu.

Baada ya saa kadhaa za kusumbuana na utingo, tulifika katika Chuo cha Ualimu cha *Nira. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia humo, sikwambii kufika Kiduni. Watu wachache walikuwa bado wamepiga foleni wakisubiri ima kusajiliwa rasmi chuoni au kuwashika mikono wana wao katika shughuli hiyo nzima. Nilijua sikuwa na kila kitu kilichokuwa kinahitajika; si vitabu si si idadi tosha ya pesa. Ile kauli ya ‘mtu hujikuna ajipatapo’, nilijua haingenifaa wakati kama huo. Nilikuwa kama mbuzi mbele ya hakimu chui! Hebu nisonge mbele kidogo… Continue reading

@DennisShonko UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

Kwa mwaka wa pili mfululizo, Tamasha ya Kiswahili iliandaliwa katika ukumbi wa Huduma ya Maktaba kwa Taifa nchini Kenya (Jumamosi, Oktoba 14, 2017) eneo la Buruburu. Ingawa sikubahatika  kuhudhuria tamasha yenyewe mwaka wa 2016, nilihabarishwa ilivyokuwa yakuigwa.

   Bw Almasi bin Ndangili—ambaye ndiye aliyeibuka na wazo la kuwapo tamasha kama hiyo, ndiye aliyenipa mwaliko. Sawa na wapenzi wengine wa lugha ya Kiswahili, nilifika mapema ukumbini licha ya kukanyaga chechele hapa na pale safarini nikiwa na mwalimu mwenzangu, Peter. Baada ya kitambo kifupi, Bw Ndangili aliyekuwa mratibu na mshereheshaji wa hafla na mwandishi wa tamthilia ya Kifo cha Mwandisi Mmachinga iliyoigizwa hapo baadaye, aliifungua warsha. Stacy alituongoza katika kuuimba wimbo wa taifa. Baadhi ya majina yakutajika yalitambulishwa kwetu k.v Swaleh Mdoe, Bi Pauline Kea, Daktari Hamisi Babusa na Profesa Kineene wa Mutiso waliokuwa wamefika mle. Continue reading