Jicho Langu

 

2. Mama Kafufuka!

__________

Kwa wanangu wapendwa,

                Natumai hamna neno. Wanangu, msiushangae ujio wangu leo. Nimeshindwa tu kuvuta subira na uvumilivu huko nilikofia. Wanangu, mmeniua mara si moja; mara mia moja au zaidi.  Mlianza kwa kunipondaponda, kunivyogavyoga, kunikanyaga, kuni… pindi wazee wenu– nasikia nao walikata roho kitambo– walipoikata mikatale ya wazungu. Mlipohakikisha sipumui tena, mkawachagua wazungu weusi niliyowazaa mimi kiasi cha kuniacha porini naliwa na wala wafu. Hamkunizika. Hebu tafakarini, mimi mama yenu aliyeishi kuwabeba mkanisahau! Ni uamuzi wenu huo, sikatai. Awaelekeze nani isipokuwa nyinyi wenyewe? Kukomaa mmekomaa, masikio na macho mmejaaliwa, ila niwatazamapo nawaona wachache wa fikra licha ya umri wenu huo mkubwa. Hashakum si matusi, akili tasa! Hata hivyo, hayo ni ya wengine, sio nyinyi mnaonisikiliza au kunisoma sasa hivi.

Najua mmeelekwa na hawa wanambee wangu. Mnavitazama visogo vyao, nanyi kwa kujua au kutojua mnaishia kunifunga sanda kwa nyendo zenu. Sikatai wapo wema kati yenu, lakini si mnajua pono mmoja akioza huoza na shazile? Uovu uzidipo huufunika wema. Hivyo basi, usomeni waraka huu pamoja. Nitaje angalau kwa kiduchu kwamba, baadhi ya mbinu na silaha mnazozitumia kunifisha kila leo ni pamoja na; ukabila, hila, wivu, umero, wizi, uchoyo, ulevi, uongo, uuaji, ubaguzi, uzembe, ufisadi… Nyingi tu! Ila leo nitakita hapa pa ‘kitu kidogo tu!’

Mama Kafufuka!

Mama Kafufuka!

Pasina shaka mnavijua virusi hivi vikitajwa huku kwangu. Goldenberg, Eurobond, NYS, Standard gauge railway (Vitaje!)…  Navyo vilianza vipi? Viliasilia wapi? Mstakabali wangu mimi na wenu wanangu utakuwa upi ikija miaka ya halafu? Mtaoza na kuozeana zaidi kama nilivyo? Swala huwa dogo kisha likawa kubwa, vivyo hivyo nanyi vitindamimba wangu, mkishakua mtakuwa kama watangulizi wenu msipotahadhari. Nami nimefufuka ili niwatahadharishe wakutahadharishwa kabla ya athari. Yanaanzia ndani yako kabla ya kuyaeneza kwa mwenzio. Yapi hapo? Kuwa mkweli. Ukiuficha ukweli, ukweli utakufichua. Aisee, kuwa na msimamo dhabiti; ukiufuata ‘upepo’ utapotea. Jitabirie kesho yako usije ukaabiri matwana ya hadi majuto. Nayo majuto ni mjukuu, huja baada ya kitendo. Zichunguze nyendo zako kwanza, usije ukachunguzwa na hali ya maisha. Tenda zuri kana kwamba  hayupo jasusi nyuma yako. Zingatia amri ya wakati usije ukatasa kabla ya kujifungulia heri ya maisha kwani ukilala, na mambo hulala na ukicheza ujanani utalipa uzeeni. Yaepuke ya kuepukwa yasije yakakupofusha. Umhudumiapo mwenzio, usimtazame kwa jicho la nje, hata kidogo! Lipe kazi jicho lako la moyoni – la nje hugilibu. Mwanangu, zijapo sheria ukazifuata, shari itaondoka. Shaka haitakukimbilia, itakukimbia. Usisahau likuondokealo lina heri nawe! Hasira zikikupanda usipende kisasi. Tumia mbinu mbadala kuibadilisha hali; ije haki. Tena mwanangu, tenda uliloratibiwa na kuandaliwa kutenda, utapendeza machoni pa wengi… Kwa ufupi, ukijiboresha utamboresha nduguyo. Mtaboreshana, wanangu. Nami niliko nitafurahia. Damu ya watangulizi wenu haitakuwa b’re. Sitajuta kuwazaa. Sitaendelea kukerwa na vicheko vya wenzangu wanichekao duniani kote.

Wanangu, kujitolea kwenu kutautoa umaskini huku kwangu. Watu wawili hawapotei njia, hivyo basi msitengane. Muungane na mtangamane ifaavyo. Msichukiane, kufanya hivyo ni kunivundisha. Sitaki nifufuliwe tena na haya yanayokirihi, mno hili la ufisadi. Katika mkao ujao (Iwapo hamtabadilika) nitawaandikia mengine kando na haya. Hatimaye, kama ishara kuwa umenielewa, mpokeze mkono aliye kando yako hapo ulipo… Ahaa! Sina jingine kwa wakati huu. N’enda zangu nikitumai hamtanifufua hivi karibuni, iwapo si kamwe.

Ni mimi mama niwapendaye,

Kenya.

_________

Mama Kafufuka!

Mama Kafufuka!

____________________

1. Jicho Langu: Our Crippled Politics.

Our Crippled Politics

Our Crippled Politics

My mind entangles a lot when I think of the political direction that we are headed to. Every politician is on the run to commercialize their deeds. Various opinions and different contentions and contagious issue that needs meticulous and serious thinking. People ignore politics at a great intensity forgetting that they are depriving themselves the sense to stand upright for their rights.

The old natives who have been in the game have made us believe that politics is indeed a dirty game but it isn’t the dirty players that ‘dirtify’ the game?

It is high time we redefine the saying that old is gold to old is copper coated with gold. For the old folks have done nothing valuable to prove the value of their age. Many of them are often after monetary values to satisfy their wobbling bellies which in the first place, are out of shape for the much they have consumed.

We need something different, the government acts like a committee. If you have been in one you could probably agree with my sentiments; A committee or a commission of enquiry that takes the longest time to generate ideas and putting them into action. Upon its judgment, nobody is contented; everybody is complaining.

Jicho Langu; Dennis Shonko

Jicho Langu; Dennis Shonko

They say that ‘too many cooks spoil the broth’. Well, I think they are spoiling the governance with the different ideologies. If Nehemiah (The one in the Bible) had chosen a committee to help him build the walls he would still be halfway.

That’s exactly why we never seem to grow economically, socially nor politically. Where is the rest of the percentage? Don’t these people realize we are growing at a decline rate? If your child could bring such a percentage of declines, wouldn’t that be a direct insult? Therefore we are being insulted, our richness and splendor, beauty and outlook.

I find it interesting that someone described a card as an art of committee generated from too many ideas defining its irregular shape.

Stabilizing our Minds.

Our Crippled Politics

Our Crippled Politics

If politics has to prosper then we have to set and stabilize our minds to succession. You have heard of people who want to be associated with rich people because they seem to have ‘rich ideas’. My perception is that, poor people even suit more. They have a wide variety of experiences ranging from best moments to worst moments. If we look at it from a status point, we are wrong. It is evident in the Holy Books – David was a mere boy who fought the Palestines while Mohammed was not of eloquent speech yet he served the people.

Wealthy people always seem to prosper, reason being we have stereotyped our minds that they have more to offer than others. It is always us to have the answer and the solution to our problems, but we can’t leakage even where the answer is too direct and common.  After all, common sense is not too common to everyone.

 

One thought on “Jicho Langu

  1. On the web Cialis kaufenalways a significant admirer of linking towards bloggers that I fairly which include still do not consider a whole lot of backlink Pretty such as in opposition to Log in just toward Respond to

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s