@DennisShonko UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

Kwa mwaka wa pili mfululizo, Tamasha ya Kiswahili iliandaliwa katika ukumbi wa Huduma ya Maktaba kwa Taifa nchini Kenya (Jumamosi, Oktoba 14, 2017) eneo la Buruburu. Ingawa sikubahatika  kuhudhuria tamasha yenyewe mwaka wa 2016, nilihabarishwa ilivyokuwa yakuigwa.

   Bw Almasi bin Ndangili—ambaye ndiye aliyeibuka na wazo la kuwapo tamasha kama hiyo, ndiye aliyenipa mwaliko. Sawa na wapenzi wengine wa lugha ya Kiswahili, nilifika mapema ukumbini licha ya kukanyaga chechele hapa na pale safarini nikiwa na mwalimu mwenzangu, Peter. Baada ya kitambo kifupi, Bw Ndangili aliyekuwa mratibu na mshereheshaji wa hafla na mwandishi wa tamthilia ya Kifo cha Mwandisi Mmachinga iliyoigizwa hapo baadaye, aliifungua warsha. Stacy alituongoza katika kuuimba wimbo wa taifa. Baadhi ya majina yakutajika yalitambulishwa kwetu k.v Swaleh Mdoe, Bi Pauline Kea, Daktari Hamisi Babusa na Profesa Kineene wa Mutiso waliokuwa wamefika mle.

Bw Ndangili aliendelea kueleza kuhusu safari ya tamasha yenyewe, yaani ilivyoasisiwa, ukuaji na inakoelekea. Hapo, aliwataja wafadhili wakuu—Taasisi ya maendeleo ya mtaala nchini (KICD) na Huduma ya Maktaba kwa Taifa nchini Kenya (KNLS).

UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

Washiriki walivitononoa vipaji vyao vilivyo. Bw Maina wa Chama cha Kiswahili Kenyatta (CHAKIKE) aligusia Kiswahili na uandishi. Aliwatia shime wakenya kuvisoma vitabu vingi kadri ya uwezo wao kwani mwenyewe keshafanya hivyo.  Juma Athman alizikariri kurasa kadhaa za riwaya ya Kidagaa Kimemwozea iliyoandikwa na Profesa Ken Walibora aliyekuwa amealikwa pia. Robi Robbery hakusahau ‘Hiki Kijiji’ kabla ya Sahibul Iman kuliongoza kundi lake kuimba wimbo wa vigelegele vya Kiswahili. Kuchengwa naye hakukosa kuwasilisha ‘Zilipendwa’ mbele ya hadhira.

           WAGENI WAALIKWA

Saa tano asubuhi hivi, Profesa Kineene wa Mutiso wa Chuo Kikuu cha Nairobi alisimama jukwaani kuwapasha wajumbe kuhusu taaluma ya Kiswahili. Kwa mapana na marefu, alifafanua manufaa yanayotokana na taaluma ya lugha hii tukufu. “Kiswahili kinalipa!” Alisisitiza.

Kwisha hivyo, zamu ya kughani na kukariri mashairi na ngonjera kuhusu mada mbalimbali ilifika. Kundi lake Sahibul iman, Alamin Somo (wa redio salaam, Mombasa), Were Juma na Rangimoto au ukipenda, Jini Kinyonga, walikora nafsi za hadhira. Mahojiano yalioongozwa na Bw Monscent Namussasi yalikuwapo. Mwanahabari Swaleh Mdoe wa Citizen TV na Munene Nyaga walikosolewa kwa jahara na waziwazi, chambilecho Profesa Ken Walibora (Taifa Leo Alhamisi, Oktoba 19, 2017).

Baada ya chamcha, wahudhuriaji walichangamshwa na kuelimshwa na maigizo ya tamthilia iliyoandikwa na Bw Ndangili. ‘Maudhui yalijikita katika masaibu ya waandishi chipukizi wa Kiswahili na mapambano kati ya Kiswahili na Sheng’. Mzee Rajab Pilau kutoka Takaungu, Kilifi alikosoa makosa ya Kiswahili akirejelea usawa wa matamshi ya Kiswahili. Kauli zingine zake ziliwaacha wengine wetu tukijikuna vichwa. Bi Pauline Kea, mwandishi wa tamthilia ya Kigogo alipokezwa kinasa sauti. Hakuyasema mengi; machache aliyoyasema yalipalilia ilhamu kwa waandishi chipukizi. Dkt Hamisi Babusa alikaribishwa na baada ya kuyasema mawili-matatu, aliketi. Ikawa fursa ya mwandishi wa Siku Njema na aliyekuwa mgeni rasmi siku hiyo. Prof Ken Walibora alianza kwa kutoa ombi la iwapo angealikwa tena, asiwe mgeni rasmi. “Wapo wengine wengi wanaoweza kuwa wageni rasmi,” alitamka. Aliwaomba watu wasome vitabu sana na wasivisome vya Kiswahili pekee; Kiingereza ni muhimu pia. Kubwa zaidi, alipinga ufifi kuwa yeye na mwandishi mwenza Said A. Mohamed huwazuia waandishi wengine kutambulika kwa kuteuliwa vitabu vyao visomwe katika shule za upili. Alitoa wito kwa waandishi chipukizi waendelee kuandika. Wasikate tamaa hata kampuni za kuchapisha vitabu zisipofanya hivyo. “Lako ni kuandika, si kuchapisha vitabu. Wasipochapisha basi watakuwa wamefeli wao,” alihitimisha.

Mwisho wa yote, Tuzo kwa walioshiriki zilitolewa. Kwisha hivyo, wahudhuriaji wakatangamana na kuondoka kwa hiari yao.

5 thoughts on “@DennisShonko UFANISI WA TAMASHA YA KISWAHILI MWAKA WA 2017—BURUBURU

  1. haki help me

    2017-12-09 15:55 GMT+03:00 | Fasihi | Literature in Africa | :

    > African Literature posted: ” Kwa mwaka wa pili mfululizo, Tamasha ya > Kiswahili iliandaliwa katika ukumbi wa Huduma ya Maktaba kwa Taifa nchini > Kenya (Jumamosi, Oktoba 14, 2017) eneo la Buruburu. Ingawa sikubahatika > kuhudhuria tamasha yenyewe mwaka wa 2016, nilihabarishwa ilivyok” >

  2. Pingback: Homepage

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s