@DennisShonko NILIVYODHALILISHWA KWA KUZUNGUMZA LUGHA YA KISWAHILI

interview

Mwalimu na wanafunzi ofisini.

Nakumbuka namna mvua ilikuwa inatunyeshea mchana kutwa tulipokuwa safarini (usiulize tulikuwa na nani. Hayo ni ya siku nyingine). Safari ya kutoka jijini Nairobi kuelekea eneo la *Kiduni. Usishangae kuwa kunyesha kwa mvua hiyo hakukuitia imani yangu baridi. Baridi iliyokusudia kutugeuza kuku aliyenyonyolewa chini ya pepo zitokazo pande zote duniani. Ninachojaribu kusema ni kwamba, nilikuwa katika safari ya kwenda kuonja kipande kingine cha maisha au bora niseme, kuandika ibara nyingine ya maisha yangu.

Baada ya saa kadhaa za kusumbuana na utingo, tulifika katika Chuo cha Ualimu cha *Nira. Ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia humo, sikwambii kufika Kiduni. Watu wachache walikuwa bado wamepiga foleni wakisubiri ima kusajiliwa rasmi chuoni au kuwashika mikono wana wao katika shughuli hiyo nzima. Nilijua sikuwa na kila kitu kilichokuwa kinahitajika; si vitabu si si idadi tosha ya pesa. Ile kauli ya ‘mtu hujikuna ajipatapo’, nilijua haingenifaa wakati kama huo. Nilikuwa kama mbuzi mbele ya hakimu chui! Hebu nisonge mbele kidogo… Continue reading