Ngulamu Mwaviro ndiye mshindi wa Tuzo ya Ubunifu 2016 miongoni mwa Miswada 86

1f

Kumi na tano bora na wadhamini ya Tuzo ya Ubunifu

Tarehe 26/04/2017 ilikuwa siku ambayo mwanahabari  Ngulamu Mwaviro (Wa shirika la utangazaji la kitaifa-KBC) alitangazwa mshindi wa Tuzo ya Ubunifu ya 2016 katika hafla iliyofanyika katika ukumbi  wa Alliance Francais jijini Nairobi.   Novela yake ya “Mkamia Maji” iliibuka mswada bora miongoni mwa themanini na sita (86) iliyokuwa imetumwa na waandishi chipukizi kutoka pembe zote nchini Kenya.

Akitoa hotuba yake fupi punde alipotangazwa mshindi, Mwaviro alisema kuwa hakutarajia hilo licha ya kuwa aliamini alikuwa ameufanyia kazi mswada huo ipasavyo. “Mswada huu ni jiwe lililokataliwa na mwashi . Kuna matbaa iliyokataa mswada huu na nikaona nijaribu bahati katika Tuzo ya Ubunifu,” aliongeza. Aidha, aliwamshukuru Mungu na kuwapongeza washiriki wote.” Kando na kutunukiwa shilingi milioni moja, mswada huo utachapishwa na Matbaa ya Sportlight na kisha uchapishwe ka Kifaransa.

sew

Ken Walibora na Dennis Shonko

Kumi na tano bora

Washiriki wengine ambao miswada yao ilikuwa miongoni mwa kumi na tano (15) bora katika vitengo vya riwaya, novela na tamthilia walitunukiwa vyeti na tuzo zingine kutoka kwa Ubalozi wa Ufaransa nchini.

Waliokuwapo kushuhudia yote, kando na washiriki na walioandamana nao, walikuwapo Bw Simon Sossion ambaye ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Matbaa ya Sportlight, Bw Joe Muganda, Afisa Mkuu Mtendaji wa Nation Media Group na Balozi wa Ufaransa nchini Kenya, Antoine Sivan. Balozi huyo  aliisifu tuzo hiyo na kuwaomba Wakenya kuienzi lugha ya Kiswahili. Wote hao ambao ndio wanaoidhamini tuzo hii, waliahidi kuendeleza wimbi hili kila mwaka na mno, kuifanya tuzo inayowashirikisha waandishi chipukizi kutoka Afrika Mashariki.

gh

Dennis Shonko na Andrew Shonko

Mwenyekiti wa jopo zima, Profesa Ken Walibora ambaye ni mwandishi mtajika duniani kote, aliwahimiza (Kwa niaba ya jopo) waandishi wa kike kujitokeza na kushiriki katika tuzo hii ambayo ndiyo kubwa zaidi, ya Kiswahili, kwa sasa inayoshindaniwa.fr

Mkamia Majià Ngulamu Mwaviro

Novela hii iliandikwa kati ya mwaka wa 2013 na 2014. Kazi hii inaangazia masuala ibuka, Yupo mtoto zeruzeru anayeponea kifo kutokana na msimamo wa babake anyejua fika sio Muumba wa kukosoa maumbile. Anakiuka shinikizo kali za jamii kwamba mwanawe auawe ili kukwepa ‘laana’.

Mwandishi anaonyesha kwamba kirima kamwe hakina nafasi; ni bidii tu itaweza kumfikisha mbali. (Swahilihub)

dsw

Tuzo ya Ubunifu 2016, Tuzo ya Ubunifu 2017, Bw Simon Sossion ambaye ni Afisa Mkuu Mtendaji wa Matbaa ya Sportlight, Bw Joe Muganda, Afisa Mkuu Mtendaji wa Nation Media Group na Balozi wa Ufaransa nchini Kenya, Antoine Sivan, Dennis Shonko, Alliance Francaise, Kiswahili, Literature Africa, Ngulamu Mwaviro, KBC, Fred Indindi, Nyariki Enock Nyariki, Riwaya, Novela, Tamthilia

3 thoughts on “Ngulamu Mwaviro ndiye mshindi wa Tuzo ya Ubunifu 2016 miongoni mwa Miswada 86

  1. Niliwasilisha mswada wangu mwaka jana (2017 ) agosti ila hadi sasa sijapata habari yoyote. Kwa yeyote anayehusika naomba kujulishwa kinachoendelea kupitia anwani yangu meme. Ramachimz13@gmail

  2. Pingback: LALA PEMA PROF. KEN WALIBORA: INGAWA UMEONDOKA, HUTAFUTIKA MOYONI MWANGU. – | Fasihi | Literature in Africa |

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s