Tamthilia ya Mtahiki Meya – Timothy M.Arege

SEHEMU I

Onyesho I.

Mstahiki Meya

Mstahiki Meya

Mchezo uanzapo, tunakutana na Waridi ambaye ni nesi na Siki ambaye ni daktari. Wote wawili wako kwenye zahanati ya Jiji. Daktari Siki anaonekana mwenye kusumbuliwa na jambo fulani; pengine matatizo ya ukosefu wa dawa zahanatini. Waridi aingiapo, wanaanza kuangazia swala la ukosefu wa dawa kwenye zahanati.

Waridi anamwambia Siki kwamba, shehena ya dawa iko bahari kuu na kwamba ingewasili baada ya siku tatu. Hii ni kwa mujibu wa Mstahiki Meya mweneyewe.

Zahanati ingepokea dawa hizo baada ya siku tatu zingine baada ya kuwasili nchini. Meya anasema wagonjwa wasubiri dawa, naye daktari anashangaa kana kwamba ugonjwa nao utasubiri.

Kutokana na mazungumzo ya Waridi na daktari Siki tunagundua kwamba, zaidi ya kukosekana kwa dawa, wagonjwa hawana pesa za kulipia huduma za matibabu. Hata hivyo, amri ni kwamba, lazima wagonjwa walipie huduma za afya kabla hazijatolewa kwao. Waridi anatetea hali hii kwa kusema kwamba nchi yao ni maskini.

Siki anapomuuliza mwenye kusema kwamba nchi ni maskini, Waridi anasema kwamba ameyasikia tu maneno hayo kutoka kwa wanasiasa, vyombo vya habari na wasomi. Siki haelekei kukubaliana naye na anashangaa kwamba ‘ameyasikia tu’. (Hii inadhihirishwa kwamba, vyombo vya habari, wanasias na wasomi wanawapotosha wananchi kwamba nchi yao ni maskini.) Pindi anaingia mama mwenye mtoto mgonjwa. Waridi anamkemea lakini Siki anampokea na kuanza kumhudumia.

Tunagundua kwamba, mtoto alikula maharage aliyoletewa na mamake kutoka anakofanya kazi; kwa Mstahiki Meya. Tunaonyeshwa hapa kwamba, jamii hii inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula; haswa pale mama huyu anakiri kwamba huwa wanakula chakula cha mbwa bila ‘dhara yoyote’. Zaidi tunaona kwamba, mtoto huyu ana tatizo la utapiamlo; ushahidi wa kuwa pana ukosefu wa lishe bora. Daktari anapendekeza mtoto alazwe kwenye wadi ya watoto na anajishughulisha kumpa huduma kwa kujitengenezea dawa ya mchanganyiko wa sukari na chumvi kwenye maji moto. Anapendekeza pia kwamba, wagonjwa wote waliolemewa walazwe hata ingawa hakuna dawa huku akisema kwamba wakifa watakufa kwa kukosa dawa lakini si kwa kukosa matumaini. Anasisitiza kwa kusema ‘ganga ganga ya mganga huleta tumaini.’

Tunapata kufahamu pia kwamba,wagonjwa hawa ni wafanyakazi wa Jiji husika.. dakatari anasema “…Asasi na wahudumiwa vyote viko chini ya Meya…” akiwa na maana kwamba, hospitali ni ya Jiji na wagonjwa ni wafanyakazi wa Jiji. Inabidi wagonjwa walazwe huku dawa zikisubiriwa. Wakati uo huo Siki anashangaa ni kwa nini Meya akatoa kauli badala ya Bwana Uchumi na Kazi; inaelekea kuna jambo ambalo linaendelea pale na wanakubaliana kusubiri ili waone yatakayotokea.

Tathmini

Kutokana na onyesho hili tunaona kwamba, jamii hii imezingirwa na matatizo mengi: kwanza kuna tatizo la ukosefu wa dawa kwenye hospitali za umma. Pia kuna tatizo la ukosefu wa uajibikaji miongoni mwa viongozi kama vile Meya. Meya anatoa kauli ambazo hazifai kama vile kwamba ni lazima wagonjwa walipie huduma za afya kabla hazijatolewa kwao.

Vile vile, kuna kutojali hali ya wananchi na haswa wagonjwa, wanatakiwa wasubiri dawa hadi zifike – ishara kwamba viongozi wao hawawajali. Waridi pia hawajibiki kazini mwake; anakuwa mkali kwa wagonjwa na pia anafuata kauli za wanasiasa bila kwanza kuzingatia maadili ya kazi yake: kuokoa maisha ya wagonjwa. Tatizo la njaa na umaskini linajitokeza wazi. Wananchi wanakula chakula cha mbwa na mabaki ya vyakula kutoka kwa matajiri.

Onyesho La Pili

Onyesho la pili latokea nyumbani kwa Mstahiki Meya. Yuko mezani huku mbele yake kukiwa na mayai na chai pamoja na vyakula aina aina. Sakafuni kuna zuliaya kupendeza. Mandhari haya ni ushahidi tosha kwamba Meya anaishi maisha ya hali ya juu nay a shibe ikilinganishwa na watu wengine Jijini. Tunamwona Meya akilalamikia ‘viyai’ alivyopewa.

Mazungumzo yake yote yanaashiria mtu mwenye maringo, kiburi na kutojali. Yeye analalamika juu ya udogo wa mayai ilhali wengine hawana hata hayo mayai. Anmwagiza Dida amwagize mwenye kuleta mayai hayo asiyalete tena. Pindi anaingiadaktari Siki, nduguye. Huyu anamtabulisha Meya kwetu kwa jina Sosi. Meya haelekei kupendezwa na jambo ili; hataki kuitwa ndugu Sosi, maana eti yeye sasa ni Meya. Siki amekuja kwa Meya kumjulisha hali ilivyo kwa wananchi na haswa kuhusiana na ukosefu wa dawa na ukosefu wa fedha za kugharamia matibabu.

Badala ya kutilia maanani maswala haya, Meya anajitia hamnazo na kuanza kusifu baraza lake kama baraza bora zaidi. Siki anamkosoa haswa kwa kujilinganisha na majirani dhaifu. Anapendekeza kuzingatia ubora zaidi ya ubora wa majirani zao. Anazidi kumsimulia Meya juu ya matatizo ya watu wao; anamwabia watu wanakufa kwa njaa na ukosefu wa mahitaji ya kimsingi. Anamtahadharisha juu ya kuwaongoza watu wenye njaa. Meya anasisitiza kwamba, wenye kumchagua ni wengi na watazidi kumchagua. Anamwambia Siki kwamba akili ni mali. Ili kuthibitisha hayo, anamwagiza Gedi kupeleka ujumbe unaoagiza idhaa ya baraza kucheza nyimbo za uzalendo kabla na baada ya vipindi maarufu.

Siki anashangaa kama kwamba watu watashibishwa na nyimbo hizo na kusema kuwa, hamna haja kuwapigia watu nyimbo za uzalendo miaka hamsini baada ya uhuru. Siki analalamikia swala la maendeleo akisema, wanatembea lakini hawaendi mbele, waenda kinyumenyume. Anamkumbusha Meya kwamba, afya bora nay a bure kwa wananchi wote ni moja kati ya malengo ya mji katika mpango wake wa maendeleo ya miaka kumi. Meya anasema kwamba wao wako na malengo ya kimaendeleo ya millennia na kwamba huo ndio muhimu. Adadai kwamba wameshaingia katika kiwango cha kimataifa na kupinga hayo ni kama kumkama samba mwenye watoto.

Siki anamkumbusha kwamba, kufikia kumi sharti kuanza na moja; kwamba kumi haifikiwi katika ombwe tupu (vacuum.) Meya anaudhika na kumwagiza Gedi kumtoa nje Siki. Kasha anaagiza asilikaribie jingo lake tena bali alione paa. Meya anaagiza kuwe na mkutano wa dharuru ofisini bila ya mwanakamati yeyote kukosa.

Tathmini

Onyesho hili linamwangazia Meya kama mtu asiyejali maslahi ya wananchi aongozao. Wao wana njaa naye ana shibe kuu kufikia kiwango cha kuangalia udogo na ukubwa wa mayai.

Hajali hali za watu wake, haswa juu ya umaskini, njaa na maradhi. Anapoambiwa kuna mtoto aliyekufa kwa njaa, anasema huyo ni mmoja na kwamba wamebaki wengi wanaomuunga mkono.

Tofauti yajitokeza wazi kati ya ndugu wawili, Siki na Sosi. Siki ni mwenye utu ilhali Sosi ana ubinafsi mwingi na kiburi.

Tofauti za kitabaka zinaonekana huku watu wa tabaka la juu wakiwa wanaishi maisha ya raha nao wa tabaka la chini wakiubeba mzigo mzito wa hali ngumu ya maisha; njaa na maradhi.

 Kutoka HAPA!

23 thoughts on “Tamthilia ya Mtahiki Meya – Timothy M.Arege

  1. Pingback: Free Piano

    • 1.Jinsi Meya anauza mali ya umma (fimbo)bila kuwajulisha wanacheneo.
      2.Kusema kuwa wagonjwa walipie pesa zahanatini ilhali dawa hakuna.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s